KNUT yamwonya Magoha kuwa walimu hawatatekeleza mtalaa mpya

Chama cha Kitaifa cha Walimu  KNUT kimemweleza  Waziri Mteule wa Elimu,  Profesa George Magoha kufahamu kuwa walimu hawako tayari kuutekeleza mtaala mpya wa elimu.

Akihutubu wakati wa uchaguzi mdogo wa viongozi wa KNUT Kaunti ya Trans Nzoia,  Naibu katibu mkuu wa chama hicho,  Clement Omolo amesema  mtaala huo umeharakishwa na kwamba walimu hawakushirikishwa  na kutayarishwa ipasavyo .

Omolo aidha ameihimiza Tume ya Huduma za Walimu, TSC kulitii agizo la Rais Uhuru Kenyatta na lile la mahakama la kuusitisha uhamisho wa walimu wakuu hadi maeneo mengine ya nchi.

Related Topics