Serikali yashauriwa kutenga Fedha zaidi kuimarisha Muundo msingi za shule

Mpango wa kuhakikisha kuwa watahiniwa wote waliofanya mtihani wa darasa la nane, KCPE mwaka jana kujiunga na shule za upili hautafanikiwa iwapo serikali haitaimarisha miundo-msingi.

Katika hoja iliyowasilishwa bungeni na Mbunge wa Emuhaya, Omboko Milemba, serikali imeshauriwa kuhakikisha kuwa asilimia 70 ya fedha zinazotengewa hasa shule za upili za kutwa zinatengewa muundo msingi.

 

Hoja hiyo imeunga mkono na wabunge ambao wanapendekeza pesa hizo kutumwa kupitia hazina ya maendeleo bunge CDF. Naibu Kiranja wa Wachache katika Bunge la Kitaifa, Chris Wamalwa amesema ukosefu wa muundo msingi katika shule nyingi huathiri matokeo ya wanafunzi katika mitihani ya kitaifa.

 

Wakati uo huo, baadhi ya wabunge wamependekeza majengo katika shule za umma nchini, kujengwa ili kuwafaa wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Akichangia hoja hiyo Mbunge maalum, David ole Sankok, amesema wanafunzi hao wamekuwa wakiathirika pakubwa kwani mahitaji yao hayashughulikiwi.

 

Haya yanajiri siku tatu tu baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuahidi kuwa fedha zaidi zitatengwa kuimarisha muundo msingi kwenye shule za umma nchini.

Related Topics