Utafiti wabainisha kwamba ni vigumu kuepuka matumizi ya mitandao ya kijamii kuliko pombe na matumizi ya dawa za kulevya

Utafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Daystar, umebainisha kwamba ni vigumu kuepuka matumizi ya mara kwa mara ya mitandao  ya kijamii kuliko unywaji wa pombe na matumizi ya dawa za kulevya. Utafiti huo uliwaohusisha watu zaidi ya 200, wenye umri wa kati ya miaka 18 na 55, ulifanyika kati ya Januari 9 na 16 mwaka huu.

Utafiti huo ulilenga kubaini uwezo wa mtu kuzuia matumizi ya mitandao kila siku. Utafiti wenyewe umebainisha kwamba ni vigumu kwa watu kuzuia matumizi ya twiter na facebook ilinganishwa na uwezo wao wa kujiepusha na unywaji wa pombe na matumizi ya dawa za kulevya.

Hulka hii ya Wakenya inakisiwa kuwachangiwa na gharama ya chini ya kutumia mitandao ya kijamii ikilinganishwa na pesa nyingi zinazohitajika ili kununua pombe na dawa za  kulevya. Kinyume na matarajio, imebainika  kwamba  Wakenya ni wepesi wa kuzuia matumizi mabaya  ya pesa, kushiriki michezo na ngono tofauti na ari ya kutumia mitandao.

Related Topics