Watu 5 wafariki dunia kwenye ajali ya ndege Turkana

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, Rubani wa Naibu wa Rais William Ruto, Mario Magonga amefariki katika ajali ya ndege kwenye Kaunti ya Turkana.

Polisi pamoja na Mbunge wa Kitutu Chache Kusini Richard Onyonka, ambaye ni binamu ya rubani huyo wamesema kuwa ndege hiyo aina ya helikopta ilitoweka karibu na Ziwa Turkana Jumapili jioni na kwamba alikuwa amewabeba abiria wanne raia wa Marekani.

Miili na mabaki ya ndege hiyo imepatikana mapema leo mwendo wa saa kumi alfajiri huku Mamlaka ya Safari zaa Ndege ikianzihsa uchunguzi kubaini kilichosababisha ajali hiyo.

Rubani huyo aliwahi kufanya kazi na shirika la Tropic Air Kenya uhadi mwezi Juni mwaka 2015 kabla ya kujiuzulu. 

Related Topics

Turkana