Aliyekuwa Seneta Maalum, Joy Gwendo apata afueni ya muda baada ya kuondolewa kifungo

Kifungo cha miaka miwili alichopewa aliyekuwa Seneta Maalum wa Jubilee Joy Gwendo kufuatia kosa la ulaghai wa shilingi milioni 1.7 kimeondolewa.

Hata hivyo hayuko huru kwa asilimia mia moja, kwani Mahakama Kuu itampa kifungo rasmi Jumatatu wiki ijayo kwani hajathibitisha kuwa hana hatia kufuatia rufaa aliyowasilisha.

Gwendo alihukumiwa na Hakimu wa Mahakama ya Ufisadi Douglas Ogot mwezi Disemba mwaka uliopita, lakini akawasilisha kesi katika mahakama kuu ambapo iliamuru aachiliwe kwa pesa taslimu shilingi laki nne. Katika uamuzi wake Jaji John Onyiengo alisema Mahakama ya Katiba ilifanya makosa kumhukumu bila ya kumpa nafasi ya faini.

Alihukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya ulaghai na utumiaji mbaya wa ofisi. Alikanaa makosa matano ikiwemo utumiaji mbaya wa ofisi, kutoa hundi bandia na kuiba.

Related Topics

Joy Gwendo kifungo