Mzungu mwenye roho ya paka

Osman Erdinc Elsek alipokua kizimbani Shanzu na wakili wake Cliff Ombeta. [Photo, Courtesy]

Ni alfajiri na mapema, siku ya Ijumaa tarehe 22 mwezi Februari 2019 ambayo mshukiwa anayedaiwa kuwa aliwalawiti wasichana wa makamu aliokuwa akiishi nao kwake nyumbani, atarajiwa kujiwasilisha kortini baada ya kikao chake cha mwisho kuachiliwa kwa dhamana.

Mlalamishi wa kesi hii ya ulawiti, twaambiwa ni shule ya kisasa ya Greenwood Academy yenye kutoa mfumo wa elimu ya kimataifa katika maeneo ya Nyali, katika kaunti ya Mombasa ambayo wasichana hawa watatu wanasomeshwa na mshukiwa. Hatahivyo, wameikabidhi idara ya usimamizi wa watoto na ile ya mahakama chini ya afisi ya mkuu wa DPP pamoja na afisi ya mkuu wa ujasusi nchini DCI kuendesha kesi hii huku shule isubiri wakati wa ushahidi kama shahidi kindumbwendumbwe hiki.

Mshukiwa anaekabiliwa na mashtaka haya ni muekezaji wa humu nchini, hususan Kilifi na Nairobi mwenye uraia wa taifa la Uturuki (Turkey), Osman Erdinc Elsek mmiliki wa kampuni inayojihusisha na ujenzi wa nyumba na biashara nyinginezo ya Elsek & Elsek Group of Companies.

Tukirudia siku hiyo ya Ijumaa ya Februari 22, 2019, huku mawakili wa pande mbile na hakimu pamoja mwendeshaji wa mahakama wa serikali na vyombo vya habari wakijiandaa kusubiri kikao cha mahakama katika korti la Shanzu (Shanzu Law Courts), daraja la Mtwapa linalounganisha kaunti ya Mombasa na Kilifi, limejaa msururu wa watu wa kila aina tulioambiwa kuwa wametokea sehemu za Mtwapa na Kikambala ambako mshukiwa anaishi na kunakotajwa kuwa chanzo cha madai aliyoshtakiwa nayo.

SEE ALSO :Three girls seek reunion with man accused of defiling them

Kwa wale ambao walikuwa mara yao ya kwanza kama mimi, nilijua leo kutawaka moto ikiwa halaiki kubwa ya wananchi wa kawaida wamefurika mahakamani kwa kesi kama hii inayowahusisha vijuza. Siyo wanawake, wanaume, watu wa rika la makamu, walemavu wake kwa waume, waathiriwa wa magonjwa wa virusi wanaoishi kwa madawa na watu wa kawaida wote walifurika kortini siku hii. Kwa kifupi, niliona hali ilivyo, hapa leo siyo kwema.

Osman Elsek. [Photo, Courtesy]

Mshukiwa mashuhuri

Kufumba na kufumbua, umati wote huo kamwe haukuwa umekuja kuandamana juu ya mshukiwa wa ulawiti bali wote, wengi wakiwa ni majirani kutoka vijiji majirani na boma lake la Kikambala, Mtwapa wamefika kuonyesha umoja kwamba wako pamoja wakati huu wa kulimbwikizwa madai hayo.

Kulingana na baadhi ya wanakijiji walioambatana naye kutoka Kikambala kumshindikiza hadi kortini wanadai kuwa kuna njama ya watu fulani na taasisi kadhaa ikiwemo shule lalamishi kuwa wanataka kumfurusha Mzungu wao ili wapore mali yake ikiwemo ardhi na majengo chungu nzima aliyonayo baada ya kujaribu kwa njia nyingine na wakashindwa.

Mnamo Ijumaa hii ya 22, mahakama ilidinda kuendelea na kesi ya Mzungu Osman Elsek na badala yake kuamuru kiongozi wa mashtaka kuihamisha hadi mahakama ya Malindi kwa sababu, mshukiwa amedhihirisha wazi kuwa anao ushawishi mkubwa katika mahakama ya Shanzu. Hii ni baada ya jaji kujionea mfuriko wa waliohudhuria kikao hicho kuwa ni wafuasi ama marafiki wa Elsek na isitoshe, yeye ni mmoja wa wadhamini waliosaidia kujengwa kwa baadhi ya majengo hayo ya Shanzu.

Kizungumkuti cha wazazi

Tulibahatika kumpata mzazi mmoja ambaye mtoto wake ni miongoni mwa wale wasichana watatu wanaosomea shule ya Greenwood Academy na anayeorodheshwa kuwa miongoni mwa waliolawiriwa na Mzungu nyumbani mwake Kikambala. Hii ni baada ya mashirika mawili ya haki za kibinaadamu kuwasilisha ombi lao kwamba kuna taskwishwi na kesi hii kuhusu umri wa wasichana husika na kizungumkuti cha wazazi wao kukatazwa kuonana na watoto wao kupitia kwa wakili wa Mombasa, Morris Mukami.

Mzazi mmoja kati ya wale watatu, pia alikamatwa siku moja kabla ya kusikizwa kwa kesi hiyo kwa madai kwamba anayo njama ya kuulegeza ushahidi baada ya kugundulika kwamba huenda wasichana wote watatu wakawa wamepita umri wa miaka 18.

Ijapo siyo wengi waliojua yaliyoendelea baada ya kikao cha Shanzu, mshukiwa Elsek alikamatwa mara moja punde tu mahakama ilipoagiza kesi kuendelezwa kule Malindi baadaye mwezi Machi. Kulingana na mashtaka mapya ambayo tulifuatilia moja kwa moja hadi korti la Kilifi ambako alifikishwa mwendo wa saa nane mchana akishtakiwa pamoja na mzazi huyo kwa madaia ya kuwa na vyeti vya watoto wawili wanaohusishwa na kesi hiyo ikiwa ni pamoja na mtoto wake.

Kulingana na mzazi huyu ambaye jina lake tumelibana, anasema kuwa wamekatazwa kuonana na watoto wao kwa sababu madai mengi ni ya uongo na kwamba yeye kama mzazi anawajua kati ya watoto hao ni watukutu na daima amekuwa akihusishwa kutatua visa kadha wa kadha. Anadai kwamba kulingana na ripoti anazozipata kama mzazi, shule husika ambayo ni ya matajiri, ameletewa malalamishi tele kuhusu anasa zinazoendelea shuleni humo.

Mahakama iliamuru uchunguzi wa umri wa wasichana hao na pia wazazi wao waruhusiwe kuonana na watoto. Ingawa hivyo, yaaminika agizo hili limewatia maafisa husika tumbo joto pamoja na usimamizi wa shule kutokana kwamba tayari mzazi tuliyezungumza naye, alithibitisha kwamba mtoto wake alitumia simu ya mtu juzi na kumwelezea kwamba kuna vihoja kwenye taarifa zao walizoshurutishwa kuandika na usimamizi wa shule.

Licha ya kesi kuendelea, usimamizi wa shule ambao uko upande wa ushahidi, ungali unawasiliana na Mzungu Elsek kwamba awalipie watoto wake (hao) watatu karo ama sivyo wafukuzwe shule.

Osman Elsek. [Photo, Courtesy]

Mzungu wa roho ya paka

Uchunguzi wa kina unabainisha ya kuwa masaibu yanayomkumba muekezaji huyu Osman Elsek huenda yakawa yamesababishwa na msimamo wake mkali dhidi yake na usimamizi wa shule ya Greenwood Academy, ambao hadi kufikia mwezi Novemba mwaka uliopita wa 2018 ulikuwa umamshawishi muekezaji huyu kuungana kwa kushirikiana kutumia kipande cha ardhi yake ya Kikambala, kuanzisha kitengo cha shule nyingine, tawi la Greenwood Academy.

Ujumbe wa shule ya Greenwood kulingana na ujasusi wetu, ukiongozwa na wakurugenzi wake watano walimpelekea Elsek pendekezo la kuwepo kwa shule tawi lao kwenye ardhi ya Kikambala itakayoitwa Kikambala Greenwood Academy kama washirika wake kwenye biashara hiyo. Kinara wa ujumbe David Mokero aliongoza vikao vya Kikambala mnamo Mei 22, 2018, Mei 29, 2018 na cha mwisho kikawa tarehe 12 Novemba 2018.

Kulingana na mndani wa suala hili katika safu ya usimamizi, sababu za kumshirikisha Mzungu huyu ni deni ambalo Elsek anadai benki moja humu nchini ambayo alishinda kesi yake ya kibiashara na kuamriwa kulipwa pesa zake. Inakisiwa muekezaji huyu ambaye ni bilionea ama mshefa wa mapeni ya kiwango cha juu kama wakili wake Cliff Ombeta anavyomtetea mahakami kuwa ni muekezaji ambaye ameezeka zaidi ya bilioni 2 humu nchini hivyo hawezi kutoroka anadai benki hiyo siyo chini ya shilingi bilioni tano.

Wakati huo huo inadai kwamba usimamizi wa shule nao ulihitaji ushirika wa kibiashara siyo tu kwa  mshukiwa bali kwa mshirika yeyote yule kwani kufikia mwishoni mwa mwaka jana, inakisiwa kudaiwa siyo chini ya shilingi 1.2 milioni ya kodi na wenye majengo waliyokodisha ya shule yao.

Mvutano wa mzungu na (PUEA)

Tunaposema kuwa mzungu huyu ana roho ya ‘Paka’ ambaye kwa wataalam husema paka huwa na maisha saba, ni kumbu kumbu zake za mivutano ya kisheria na jinsi alivyoweza kupitia katikati mwa tundu ya sindano.

Mnamo Mwezi June tarehe 20 mwaka 2012, Osman Elsek alipata kichapo cha ugonjwa wa moyo baada ya kufahamishwa kwamba Chuo Kikuu cha Presbyterian University of East Africa (PUEA) kilicho na makao yake Thogoto, kimedinda kumlipa pesa zake shilingi 226 milioni. Kulingana na taarifa za The Standard ambazo zilinukuu habari hizi, alilazwa kwa muda wa wiki mbili katika hospitali ya Aga Khan kwa mshtuko.

Sawa na jinsi usimamizi wa shule ya Greenwood walivyotaka, Elsek alikuwa ameelewana na chuo hiki kwa mkataba maalum wa BOT (Buy, Operate and Transfer) kwamba jenga usimamie kwa muda kabla ya kuregesha umiliki chini za kanuni ya maelewano yaliyopo baina ya muekezaji na mshirika. Kampuni ya Elsek baadaye ilikuwa ilipwe milioni 89 kwa kipindi cha miezi 40. Alitakiwa kumaliziwa deni lake kufikia mwezi Oktoba tarehe 28 mwaka 2014 lakini wapi hajaziona kamwe.

Kufikia sasa Elsek alishinda kesi yake dhidi ya chuo kikuu cha PUEA kwa mujibu wa maktaba ya mahakani kwamba anadai siyo chini ya bilioni 3 ambayo korti ilamuru alipwe. Wandani bado wanashirikisha mwiba huu na kesi ya sasa kwa kuwa wafuasi wa kanisa hilo lenye usimamizi wa chuo hali kadhalika wanao uhusiano wa karibu na shule inayozungumziwa. Yaaminika mzungu ameshaumwa na nyoka mbeleni na hivi sasa akiona ukambaa ama ukoka wa nyasi anaruka!

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

ElsekMtwapa