Wiper kuwatema wanachama waliokiasi chama hicho

Na Carren Omae

Gavana wa Machakos, Alfred Mutua, Wabunge Regina Ndambuki, Joe Mutambu, John Munuve na  Kisoi Munyao watafurushwa, kwa kuviunga mkono vyama vingine vya siasa.

Kamati ya nidhamu ya Chama hicho imependekeza wanachama wake waliokiasi chama hicho kuondolewa chamani rasmi. Kwenye ripoti ya uchunguzi iliyowasilishwa kwa Naibu mwenyekiti wa chama hicho Mutula Kilonzo Jr, Kamati hiyo imesema imebainisha kwamba wanachama hao walikiuka sheria za chama kwa kuvipigia debe vyama vingine.

Ripoti hiyo inasema kwa kuzingatia ushahidi uliowasilishwa na mawakili wa wanacahma hao, ni wazi kwamba wamejiondoa chamani.

Kamati hiyo aifdha imemlaumu Gavana Alfred Mutua vile vile kwa chama chake cha siasa cha Maendeleo Chap Chap hivyo hatua inayokwenda kinyume cha sheria.

Sasa baraza kuu la wajumbe wa chama linatarajiwa kukutana Jumatatu kujadili ripoti hiyo na iwapo itaidhinishwa iwawasilishwa katika kamati kuu ya chama ili itekelezwe.