Mahakama yakataa kuwaachilia kwa dhamana washukiwa wa mauaji ya wakili Willy Kimani

Na Suleiman Yeri

Mahakama Kuu imekataa kuwaachilia kwa dhamana maafisa wanne wa polisi wanaohusishwa na mauaji ya Wakili Willie Kimani, mteja wake na dereva wa teksi.
Jaji Jesie Lesit amesema kuna uwezakano mkubwa wa washukiwa hao, Fredrick Leliman, Leonard Mwangi, Silvia Wanjiku na Stephen Cheburet kutatiza uchunguzi na kutishia mashahidi.
Aidha ameongeza kuwa baadhi ya mashahidi hao ni jamaa za Kimani na iwapo watafahamu wanne hao wapo huru basi hawatatoa ushahidi kwa kuhofia maisha yao.
Maafisa hao wanne wa polisi sasa wataendelea kuhudhuria vikao vya kesi dhidi yao wakiwa korokoroni. Wamekuwa wakizuiliwa tangu walipotiwa mbaroni mwezi Agosti.
Mwili wa wakili Kimani na Mteja wake na dereva wa teksi ulipatikana umetupwa katika msitu wa Kilamambogo ukiwana majeraha ya kupigwa kwa silaha butu.