×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Jicho pevu: Je Seneta Muthama alikosea, ama ni vile aligusia jina la Waiguru?

News
 WanaCord walipokuwa katika uwanja wa Uhuru Park

Wanadamu wapo wa aina tatu. Wa kwanza ni kama chakula huwezi kumwepuka. Wa pili ni kama dawa unamtafuta unapomhitaji na wa tatu ni kama maradhi humuhitaji kabisa. Kati ya hawa watatu kuna aina mbili ya wafuasi wao; mashabiki na wanafiki. Hakika lugha inayoeleweka vyema na wapiga kura ni lugha ya Kiswahili.

Je, Seneta Muthama alikosa? La. Muthama alitumia Kiswahili ipasavyo kutoa mfano. Hamna chuki katika matamshi yake ila ukweli mtupu. Wanajubilee walisahau kuwa kuna tofauti ya kubofya embe na kutomasa embe. Ama ni kwa vile aligusia jina la Anne Waiguru kutoa dukuduku zake kwa kutumia lugha ya kisanii?

Muthama alitaka tu kujua ubora wa Waiguru akilinganishwa na wenzake waliochukuliwa hatua za kisheria au wanaosubiri hatma zao wakiwa nje ya serikali. Muthama alimaanisha kwamba serikali ya Uhuru itaondolewa mamlakani na wafisadi wake wote siku hiyo ikifika wataandamana naye hadi Gatundu.

Joseph Nkaissery

Nkaissery alikosea alipoamuru Seneta Muthama aandikishe tarifa na idara ya upelelezi. Bwana Nkaissery, alichofanya Muthama ni kucheza na maneno na ulichofanya wewe ni kucheza na siasa. Sisemi Muthama ni malaika hana kosa lolote tangu azaliwe, bali ninachojaribu kukueleza Bwana Waziri ni kwamba Wakenya hawana muda wa kupoteza na maswala yasiyo na faida.

Majuzi mtoto mdogo wa miaka kumi na sita hivi kama sijakosea, aliuawa na afisa wa polisi huko Thika. Familia ya msichana mdogo aliyeuawa huko Mombasa kwa jina la Kwekwe Mwandaza bado hawajapata haki yao. Wal’omuua Meshack Yebei bado wako huru, vituo vya polisi vimekuwa vituo vya uwekezaji. Huwezi kusaidika katika vituo vya polisi bila pesa. Sheria zimekuwa zenye dhuluma, kushikwa na kudhulumiwa ndio maisha ya kila siku ya Wakenya. Haya ndio mambo wizara yako inafaa kutilia umuhimu.

Jeshi la hashtag #IstandwithWaiguru #RespectthePresidency. Mambo gani haya jameni! Mimi nitasimama na Wakenya. Tusitumike tu kufanikisha upambe na uumbaji, la sivyo tutawafanya wananchi wawe masikini na kuwanyima nafasi ya mwamko wa kisiasa.

Itawezekanaje wananchi kuwaheshimu wanasiasa wasiowaheshimu. Wanasiasa wanaojigamba kuwa ‘waheshimiwa’ ama ‘watukufu,’ almuradi wajitofautishe na wengine. Wanachapisha picha kwenye kanga za akina mama, zinazopepea kwenye sehemu ya makalio. Hii ndio mbinu ya hashtag battalion. Mbinu ya upambe wa ‘mfua bati’ kama alivyosema Shabaan Robert katika shairi lake.

Tuepuke uongozi sawia na ule wa aliyekuwa Rais wa Zambia Frederick Chiluba ambaye licha ya yeye kujifanya ‘mlokole’ wakati wa utawala wake, aliondoka madarakani akifuatwa na kashfa nzito za uhujumu wa nchi.

Tusijipige vifua katika mitandao ya kijamii kutumia hashtag zisizo na maana. Hebu tukumbukeni kuwa penye nia njema pana mwisho mwema, penye watu wema daima pana neema na penye wema, hapakosi mema.

Mohammed Ali ni Mhariri Mkuu wa Kitengo cha Upekuzi KTN. Wasiliana naye kupitia [email protected]; [email protected]; FB: Official Jicho Pevu with Mohammed Ali ama Twitter: @mohajichopevu

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles