Amina Mohamed kuwa mwenyekiti mpya wa AU

Na Mike Nyagwoka

Kongamano la COMESA lililohudhuriwa na viongozi kutoka mataifa kumi na manane, limeafikia uamuzi wa kumuunga mkono Waziri wa Masuala ya Kigeni, Amina Mohamed kuwa Mwenyekiti wa AU.

Mataifa hayo vilevile yameomba uungwaji mkono kwa Yacin Elmi Bouh wa taifa la Djibouti kuwa Naibu Mwenyekiti wa AU.

Uwezekano wa Amina Mohamed kutwaa wadhifa huo unaendelea kuimarika huku Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto wakiendelea kumpigia debe.


Mataifa ambayo kufikia sasa yamemuunga mkono Balozi Amina ni Burundi, Comoros, DR. Congo, Djibouti, Misri, Eritrea, Ethiopia, Libya, Madagascar, Malawi, Mauritius, Rwanda, Ushelisheli, Sudan, Uswizi, Uganda, Zambia na Zimbabwe.