Ripoti kuhusu sababu za kuteketezwa kwa shule kuwasilishwa kwa Matian'gi

Muda mfupi tu baada ya Waziri wa Elimu, Fred Matiang'i kujumuika na wabunge mbalimbali wa Kaunti ya Kisii kwa hafla ya kuchanga fedha katika Shule ya Upili ya Wavulana ya Nyamache Jumatatu, tukio jingine la mabweni mawili kuteketezwa usiku wakuamkia Jumanne limeripotiwa shuleni humo.
Kufuatia hali hiyo OCPD wa Nyamache, Japhet Mwiricha amesema maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi wa kubaini chanzo cha moto huo.
Kauli hii inajiri wakati washikadau katika sekta ya elimu wakitaka ripoti ya uchuguzi kuhusu msururu wa uteketezaji wa shule kuwekwa wazi kwa umma.
 
Maafisa wa usalama na wale wa elimu wanatarajiwa kuwasilisha ripoti yao Jumatano kwa Waziri Matiang'i.
Wakati uo huo Seneta wa Nyamira, Kennedy Mongare amekashifu hatua ya Matiang'i kuamuru wazazi walio na wanafunzi katika shule zilizoteketezwa kugharimia hasara iliyoshuhudiwa.

Na , Sulleiman Yeri

Related Topics

fred matiangi