Please enable JavaScript to view advertisements.
×
App Icon
The Standard e-Paper
Stay Informed, Even Offline
★★★★ - on Play Store
Download App

Wanafunzi walioteketeza shule kutosajiliwa katika shule nyingine asema Matiang'i

Waziri wa Elimu Fred Matiang'i amewaagiza wakuu wa shule za umma kutowasajili wanafunzi kutoka shule ambazo zimeteketezwa siku za hivi karibuni.  Matiang'i amesema hatua hiyo itasaida kuhakikisha wanafunzi waliohusika kwenye uharibifu wa mali katika shule zao wanawajibishwa. Amesema sharti wahusika wawasilishe barua kutoka kwa wakurugenzi wa elimu kwenye kaunti zao kabla ya kuruhusiwa kusajiliwa katika shule yoyote ile.
Wakati uo huo amewataka wanafunzi kutafuta njia mbadala za kuwasilisha malalamiko badala ya kuharibu mali shuleni. Vilevile ametoa makataa ya hadi Jumatano kwa wakuu wa elimu katika maeneo ambayo shule zimeteketezwa kuandaa ripoti kuhusu vyanzo vya visa hivyo.
Ameyasema haya baada ya kuizuru Shule ya  Tengecha na ile ya Itierio ambazo mabweni yaliteketezwa na wanafunzi.

Na, Beatrice Maganga

Premium Article

Get Full Access for Ksh299/Week.

Fact-first reporting that puts you at the heart of the newsroom. Subscribe for full access.
Continue Reading  →
What you get
  • Unlimited access to all premium content
  • Ad-free browsing experience
  • Mobile-optimised reading
  • Weekly newsletters & digests
Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payments Kenya's most trusted newsroom since 1902
Support Independent Journalism

Stand With Bold Journalism.
Stand With The Standard.

Journalism can't be free because the truth demands investment. At The Standard, we invest time, courage and skills to bring you accurate, factual and impactful stories. Subscribe today and stand with us in the pursuit of credible journalism.

Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payment Kenya's most trusted newsroom since 1902

Follow The Standard on Google News

Related Topics

fred matiang’i