×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Maisha Peupe: Kamilisha mbio yako ya maisha bila woga

News
 Kamilisha mbio yako ya maisha. Picha: Hisani

Maisha ina misimu. Misimu hii mara nyingi hutuletea majukumu tofauti tofauti kama binadamu.

Majukumu haya huanza kutuandama pale tunapozaliwa, na hufululiza hadi tunapokuwa watu wazima.

Huenda majukumu hayo yametengwa na jamii, familia au pia zile za kibinafsi.

Kwa haya yote, itahitajika kujitolea kwako kwa hali na mali. Huenda ukahitajika kutoa wasaa wako, nguvu zako au hata mawazo yako ili kuyatimiza malengo yako.

Hata hivyo, barabara tunayoifuata kuafikia malengo yetu mara nyingi huwa imesombwa na matatizo sio haba. Kwa mfano, leo nimeamua kupunguza uzito wangu wa mwili. Kwa hivyo, imenibidi kufanya mazoezi ya dharura huku nikitilia maanani lishe bora.

Ninafanya kila niwezalo kufanikiwa baada ya kipindi fulani. Safari hii sio rahisi. Wakati mwingine nimejipata nikila zaidi chakula ambacho sifai kula. Wakati mwingine mazoezi yanakuwa magumu, kwani inagharimu nguvu, muda na kujitolea kuusukuma mwili wangu ili kupunguza kilo.

Watu wengi wanamazoea ya kukata tamaa hata baada ya kuwekeza fedha na wakati ili kukamilisha malengo fulani.

Huenda ikawa ni biashara, masomo au jambo lolote lile lenye manufaa kwako.

Wengi pia hukata tamaa pale wanopokumbana na majaribio mbali mbali ambayo huja kwa ghafla.

Ningependa kuwahimiza Ijumaa ya leo ya kuwa licha ya pandashuka ambazo zitakukuta unapoazimia kutimiza malengo yako, kamwe usikate tamaa.

Kila unapoanzisha jambo, hakiisha umeikamilisha.

Wanaozawadiwa maishani sio walioanza jambo, bali waliostahimili joto, maumivu na mateso ili kukamilisha walioafikia kuyafanya na ndiposa wakaitwa washindi.

Mfano mzuri ni ule wa mashindano ya marathon ya Olimipiki huko Rio, Brazil. Licha ya kuwa mashindano haya yalikuwa magumu, huku washindi watatu pekee wakipokea zawadi, wengi walijikakamua na kukamilisho mbio zile. Hicho ndicho kilele cha mashindano. Kwa hivyo, ni sharti ujikakamue  kukamilisha jambo.

Wasiliana nami

[email protected]

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles