MamadouMamadou Sakho ameondolewa lawama za utumizi wa dawa za kusisimua misuli

Na,Hassan Ali

Beki wa Liverpool Mamadou Sakho mwenye umri wa miaka 26 ameondolewa lawama za utumizi wa dawa za kusisimua misuli baada ya Chama cha kupambana nadawa hizo WADA kuachia mbali kukata rufaa ya shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA, lililosema kuwa mchezaji huyo hakutumia dawa hizo.