Bodaboda wachangia kuongezeka kwa ajali

Na, Sophia Chinyezi

Wahudumu wa bodaboda wametajwa kuwa chanzo kikuu cha ajali za barabarani nchini, huku vifo mia tatu thelathini na nane vikiripotiwa tangu mwanzano mwa mwaka huu. Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Uchukuzi na Mamlaka ya Usafiri na Usalama Barabarani NTSA, wahudumu hao huchangia asilimia ishirini ya vifo nchini kila mwaka.
Haya yameibuka wakati wa uzinduzi wa mpango wa Rapid Results Initiative kuhusu sheria za bodaboda za mwaka 2015. Hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Kihoto mjini Naivasha.
Kwa mujibu wa Katibu wa Wizara ya Uchukuzi Irungu Nyakera, kufikia sasa, watu takribani mia sita wameaga dunia nchini kupitia ajali. Irungu aidha ameelezea wasiwasi kufuatia kuongeza kwa visa vya ajali na kusema kuna haja ya suala hilo kutatulia kwa haraka.