A woman lynched for eating human flesh-Swahili

Uchungu wa mwana aujuae ni mzazi. Msemo huu ulikuwa kama kinaya huko lugari pale mama wa watoto wanne alipouawa kwa njia ya kutatanisha kwa madai alikuwa akiwala nyama ya binadamu, hasa watoto. Wenyeji walivamia nyumba ya mama huyo maria nanjala na kuiteketeza moto, kabla ya kumkatakata kwa panga. Alifariki baadaye katika zahanati mmoja. Majirani pia walidai mama huyo alijaribu kumla nyama mwanawe. Mkuu wa wilaya ya lukuyani hata hivyo alikanusha madai hayo akisema mtoto wa mama huyo alikuwa amelazwa hospitali kitale.