×
App Icon
The Standard e-Paper
Kenya’s Boldest Voice
★★★★ - on Play Store
Download App

Kajwang Awataka Wakenya Kudukaa Vitambulisho Vipya

Wakenya wote walio na vitambulisho vya zamani wataruhusiwa kujiandikisha kama wapiga-kura ili kushiriki katika kura ya rasimu ya katiba inayotarajiwa hivi karibuni. Uamuzi huu umetangazwa na waziri wa uhamiaji Otieno Kajwang baada ya kutumiwa maombi na tume ya muda ya uchaguzi IIEC. Kajwang’ hata hivyo alisema walio na vitambulisho vya zamani hawataruhusiwa kujisajili kushirikia katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2012. Wakati huo huo zoezi la kuwasajili wapiga kura kwenye eneo bunge la mvita lilitibuliwa na maafisa wa polisi pale mwanawe aliyekuwa mbunge wa eneo hilo, Abduswamad Shariff Nassir alipojaribu kuongoza zoezi hilo, huku maafisa wa polisi wakitaja mkusanyiko huo kama usio halali na kuwatawanya kwa kutumia vitoa machozi.

Get Full Access for Ksh299/Week.
Uncover the stories others won’t tell. Subscribe now for exclusive access
  • Unlimited access to all premium content
  • Uninterrupted ad-free browsing experience
  • Mobile-optimized reading experience
  • Weekly Newsletters
  • MPesa, Airtel Money and Cards accepted
Already a subscriber? Log in