Huenda mwanaharakati Boniface Mwangi na mbunge mmoja nakuru wakakamatwa na polisi

Polisi mjini Nakuru wameitaka koti kutoa kibali cha kumkamata mwanaharakati Boniface Mwangi kwa kukaidi ombi la kuhudhuria kiakao cha koti ili kujibu mashtaka dhidi yake.

BW Mwangi ambaye sasa anawania kiti cha ubunge eneo bunge la Starehe walishtakiwa pamoja na mbunge wa Nakuru mjini masharikin David Gikaria kwa madai kuwa walibomoa ukuta wa ua la kampuni ya ENSE wenye thamani ya Sh13 milioni.

Kiongozi wa mashtaka kwenye kesi hiyo Hillary Songoyo Jumatatu alisema kuwa Bw Mwangi pamoja na Gikaria wamekuwa wakiweka vizingiti kwenye koti ili kuchelewesha kuamuliwa kwa kesi.

 “Sababu kila mara huwa ni Mwangi alisafiri na hayuko nchini au Gikaria ni mgonjwa. Walalamishi wamechoshwa na kuhairishwa kwa kesi na tunaiomba koti hii itoe kibali cha kuwakamata wawili hao,” alisema Songoyo.

Bw Pascal Mbeche, ambaye ni wakili wa mwanaharakati huyo aliifahamisha mahakama kuwa Bw Mwangi alikua amesafiri hadi nchini Zimbabwe huku akiitaka kesi hiyo kusitishwa kwa sababu Bw Gikaria pia alikua mgonjwa.

Wakili huyo alikua na stakabadhi zilizodhibitisha kuwa mbunge huyo alikua akipokea matibabu Nairobi hospital.

Wawili hao wanadaiwa kuhamasisha vijana ili wakabomoe ukuta huo mwaka uliopita kwa madai kuwa kampuni hiyo ilikua imetua kipande cha ardhi kinachaodaiwa kuwa mali ya shule ya msingi ya Naka.

Mashahidi watano waliojitokeza kwenye koti hawakuweza kutoa ushahidi wao huku hakimu mkuu Geofrey Oduor akiidhinisha ombi la kampuni hiyo kutaka kuhamisha kesi hiyo kwa mahakama nyingine.

Related Topics

Boniface Mwangi