Mgombea apanda punda akijiwasilisha kwa IEBC Nyamira

Mwaniaji wa Useneta katika kaunti ya Nyamira kwa Chama cha Democratic Party, DP, Adams Mochenwa amewashangaza wengi baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Tume ya Uchaguzi IEBC akiwa amepanda punda ili kuidhinishwa kuwania nafasi hiyo.
 
Kijana huyo, Adams mwenye Umri wa miaka 25 amesema amelazimika Kupanda punda ikiwa ni njia mojawapo ya kudhihirisha unyenyekevu, amani na kujitolea kwake kwenye Shughuli ya utoaji huduma kwa wakazi wa kaunti hiyo.
 
Mochenwa ambaye ni mhandisi wa ujenzi wa barabara, amesema fedha ambazo angetumia katika msafara wake atazielekeza kwa wakfu wake ili kuwasaidia watu wasiojiweza kando na kuwalipia karo wanafunzi wanaotoka familia maskini.
By Associated Press 7 minutes ago
Football
VAR denies Man but not Bayern in 2-0 win over Wolfsburg
Rugby
Rugby: Impressive Kenya Lioness fall short in World Challenger Series
Rugby
Rugby: Why Shujaa star Oscar Dennis retired at the age of 29
By Charles Odero 7 hours ago
Motorsport
How Formulae One Hamilton enjoyed his holiday in Kenya