Timu za Raga ‘Chipu’ na ‘Simba’ zaimarisha maandalizi

VIDEO COURTESY: 

Kama zilivyoponzwa timu nyingi za michezo nchini, mipango ya timu ya taifa ya raga ya Chipu na timu ya taifa ya wachezaji 15 kila upande imetibuliwa na janga la virusi vya Korona.

Kwa timu ya Simba, ndoto za kuvuna matokeo bora mwaka 2020 zimeingia doa licha ya kuimarisha maandalizi yao. Baada ya kutaradadi mwaka jana kwa kuinyuka namibia kwenye fainali-chipu walikuwa na hamu ya kungaa kwenye kombe la Barthes liliratibiwa kuandaliwa kuanzia tarehe 19 hadi 26 mwezi Aprili na kuahirishwa kwa kisirani cha Korona.

Ingawaje, changamoto hiyo imewapa motisha zaidi chipukizi hawa ambao umri umeanza kuwapa kisogo.

Kikwazo kingine kwa timu hii ni maandalizi ya pamoja haswa baada ya utangamano kupingwa marufuku michezoni wakati huu. Wachezaji wa timu hii kwa sasa wamepewa mpango maalum wa kufanya mazoezi ya kibinafsi wakisubuiri muelekeo.

Licha ya yote haya timu hii inaamini fika kwamba hakuna tatizo la kudumu wa changamoto milele wakiamini siku njema itaangaza tena.

Geoffrey Okwach (center) of Kenya battles with a Zimbabwe player during the Victoria cup match at Nakuru Athletics Club in Nakuru on September 21, 2019 [Photo by Kipsang Joseph/Standard]
Athletics
Were out to prove his dominance at Kip Keino Classic
Athletics
Eldoret City Marathon stars have gone ahead to rule global contests
Hockey
SCHOOL: Musingu and Tigoi Girls show their class in schools hockey
Athletics
Hellen Obiri leads Kenya's Boston Marathon sweep