Gumzo na Mwanaspoti Podcast: Ibrahim Kipkemboi Hussein; ubaguzi wa rangi umepungua Ulaya
Published Jan. 31, 2022
00:00
00:00

Bingwa mara tatu wa mashindano ya Boston Marathon, Ibrahim Hussein anasema ubaguzi wa rangi umepungua ikilinganishwa na miaka ya awali. Katika mahojiano na Mwanahabari wetu Ali Hassan Kauleni, Hussein ambaye alikuwa Mwafrika wa kwanza kushinda mbio za New York Marathon mwaka 1987 anasema ulikuwapo ubaguzi wa rangi kutoka kwa mashabiki na hata waandalizi wa mashindano.