×
App Icon
The Standard e-Paper
Fearless, Trusted News
★★★★ - on Play Store
Download App

Mili ya wanamziki yapatikana

Idadi ya mili ya wanamziki wa bendi ya  Wuod Awasi Music Group iliyopatikana kufikia sasa ni mitatu. Mili mingine sita bado haijapatikana. Mili miwili imepatikana leo asubuhi huku mmoja ukipatikana mchana. Shuguli ya kuitafuta mili hiyo inaongozwa na Mamlaka ya Masuala ya Baharini.
Kwa siku ya tatu sasa jamaa na marafiki wa wanamziki hao wamekuwa wakikita kambi kando ya Ziwa Victoria huku juhudi za kuitafuta mili hizo zikiendelea.
Wanamziki wanane wa bendi hiyo ya Wuod Awasi Music Group hata hivyo waliponea kwenye ajali hiyo iliyotokea Jumamosi wakati walipokuwa wakielekea  katika Kisiwa na Ndeda.
Waziri wa Michezo Hassan Wario amezihakikishia familia za waathiriwa kwamba serikali itazipa usaidizi inazohitaji.

Na, Beatrice Maganga

Get Full Access for Ksh299/Week.
Bold Reporting Takes Time, Courage and Investment. Stand With Us.
  • Unlimited access to all premium content
  • Uninterrupted ad-free browsing experience
  • Mobile-optimized reading experience
  • Weekly Newsletters
  • MPesa, Airtel Money and Cards accepted
Already a subscriber? Log in

Related Topics

DROWNING