Matokeo ya uteuzi wa ugavana Kaunti ya Homa Bay na Migori wafutiliwa mbali

Na Mate Tongola


NAIROBI, KENYA, Bodi ya Kitaifa ya Chama cha ODM imefutilia mbali matokeo ya uteuzi wa kinyang'anyiro cha ugavana kwenye Kaunti za Homa Bay na Migori.


Chama hicho aidha kimebuni kamati ya watu watatu kuchunguza madai ya udanganyifu na rabsha zilizoshuhudiwa wakati wa shughuli hiyo.


Hatua hii inajiri saa chache tu baada ya Gavana wa Migori, Okoth Obado kutangazwa mshindi wa uteuzi huo, na muda mfupi baadaye, mpinzani wake Ochilo Ayako akajitangaza mshindi.


Katika mkutano na wanahabari, Ayako anasema alichukua hatua hiyo baada ya maajenti wake kuthibitisha kuwa aliibuka mshindi kwa kura nyingi kumshinda Obado.


Obado alitangazwa mshindi kwa kura elfu kumi na saba, mia tisa hamsini na saba huku Ayako akipata kura elfu kumi mia sita sabini na sita.

 

Related Topics