×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Rais awaaagiza polisi kupanda miche

News

Rais William Ruto amewataka maafisa wa polisi nchini kupiga jeki kampeni ya upanzi wa miche ili kukabili athari za mabadiliko ya hali ya anga.

Akizungumza katika hafla ya kufuzu kwa makurutu katika Chuo cha Mafunzo ya Polisi wa Utawala AP bewa la Embakasi, rais ameeleza haja ya Idara vya Polisi kushirikiana na taasisi nyingine za serikali katyika uhifadhi wa mazingira.

Kama njia mojawapo ya kuanzisha kampeni hiyoi, Rais Ruto amewataka makamanda kuhakikisha miche milioni kumi inapandwa katika kaunti ya Nairobi pekee.

Vilevile, rais ametumia fursa hiyo kukariri kwamba serikali imeviwezesha vitengo vya usalama vimewezeshwa ili kukabili ujambazi, ujangili na uhalifu nchini kote.

Naibu wa Rais Rigathi Gachagua kwa upande wake amesisitiza wito kwa maafisa wa polisi kujiepusha na siasa, ili kuwatumikia raia bila mwegemeo.

Akihutubu wakati wa hafla hiyo ya kufuzu kwa makurutu 1085, Inspekta Mkuu wa Polisi IG, Japheth Koome alisema maafisa hao wako tayari kuwatumikia Wakenya bila uoga wala mapendeleo.

Awali Rais Ruto aliwatuza makurutu waliotia fora katika mafunzo ya maafisa wa polisi wa utawala.

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni kama vile Waziri wa Usalama wa Ndani ya Nchi Kithure Kindiki, Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja na makatibu wa wizara mbalimbali.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week