×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

IPOA yaunga mkono juhudi za Rais William Ruto

News

Mamlaka ya Kutathmini Utendakazi wa Maafisa wa Polisi, IPOA imetilia mkazo juhudi za Rais William Ruto kuhakikisha kwamba maafisa wa polisi waliotumia vyeo vyao kuwadhulumu raia wanaadhibiwa.

Katika kikao na Wanahabari, Mwenyekiti wa IPOA Anne Makori ameapa kuhakikisha kwamba hakuna kisa cha polisi kumdhulumu mtu kinakosa kuchunguzwa na adhabu kutolewa.

Mamlaka hiyo pia imesema kuwa itamchunguza Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi, George Kinoti ambaye aliyejiuzuu endapo atahusishwa katika uchunguzi wao.

Hata hivyo, imesema haina uwezo wa kumchunguza Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta iwapo atahusishwa na madai hayo.

Kauli ya Makori inajiri wakati ambapo maafisa wanne wa DCI tayari wameanza kuwajibishwa kufuatia kuuliwa kwa watu wawili wenye asili ya kihindi na dereva wao wa teksi.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week