Please enable JavaScript to view advertisements.
×
App Icon
The Standard e-Paper
Fearless, Trusted News
★★★★ - on Play Store
Download App

Idadi ya watu walioaga dunia kufuatia ajali ya Mwembeni imefikia, 21

Idadi ya watu waliofariki dunia kufuatia ajali katika eneo la Mwembeni, kwenye Barabara Kuu ya  Mombasa - Nairobi imefikia 21. Mtu aliyefariki ni mmoja miongoni mwa wawili waliozwa katika Hospitali ya Mariakani kwenye Kaunti ya Kilifi baada ya kuhusika kwenye ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 20 jana.  

Aidha imebainika kwamba dereva wa trela lililogongana ana kwa ana na matatu na kusambabisha ajali hiyo alitibia katika kliniki ya Bomu katika Kaunti ya Mombasa kisha kuruhusiwa kuenda nyumbani.

Ripoti ya Kituo cha Polisi cha Taru ambayo Radio Maisha imefanikiwa kuipata inabainisha kwamba Willy Musyoka alipata jeraha dogo kwenye mguu wake wa kushoto na alitoweka baada ya ajali hiyo.

Hayo yanajiri huku Pamela Chea mwenye umri wa miaka 21 ambaye alijeruhiwa vibaya kufuatia ajali hiyo akindelea kutibiwa katika Hospitali ya Mariakani katika Kaunti ya Kilifi.

Pamela  alivunjika miguu wakati wa ajali.

Premium Article

Get Full Access for Ksh299/Week.

Uncover the stories others won't tell. Subscribe now for exclusive access.
Continue Reading  →
What you get
  • Unlimited access to all premium content
  • Ad-free browsing experience
  • Mobile-optimised reading
  • Weekly newsletters & digests
Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payments Kenya's most trusted newsroom since 1902

Follow The Standard on Google News

Related Topics

Ajali, Kiembeni