Please enable JavaScript to view advertisements.
×
App Icon
The Standard e-Paper
Smart Minds Choose Us
★★★★ - on Play Store
Download App

Ukame mkali umeacha zaidi ya Wakenya milioni mbili wakikabiliwa na njaa

Vocalize Pre-Player Loader

Audio By Vocalize

Mwanamke katika kaunti ya Turkana akiwalisha mbuzi wake matunda ya porini. [Picha: Daniel Irungu]

Ukame mkali umeacha zaidi ya Wakenya milioni mbili wakikabiliwa na njaa, huku jamii za wafugaji katika eneo la Kaskazini Mashariki zikionekana kuathirika zaidi, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Maeneo ya mpakani mwa Kenya na Somalia yameshuhudia taswira za kusikitisha za mifugo waliodhoofika na kufa kwa kukosa malisho na maji, hali inayodhihirisha kwa uwazi athari za mabadiliko ya tabianchi katika Ukanda wa Pembe ya Afrika.

Kwa miaka ya hivi karibuni, misimu ya mvua imekuwa mifupi na isiyotabirika. Jamii zinazotegemea kilimo cha mvua na ufugaji zimejikuta zikikumbwa mara kwa mara na vipindi virefu vya ukame, ambapo mifugo huwa waathirika wa kwanza. Vifo vya sasa vya mifugo vinafanana na janga la kati ya mwaka 2020 hadi 2023, ambapo mamilioni ya wanyama walikufa nchini Kenya, Ethiopia na Somalia. Wakati huo, tishio la njaa kali nchini Somalia liliepukwa kwa taabu kupitia msaada wa haraka wa kimataifa.

Ukanda wa Pembe ya Afrika umekumbwa na misimu minne mfululizo ya mvua zisizotosha. Kipindi cha mvua ya Oktoba hadi Desemba kimeripotiwa kuwa miongoni mwa misimu mikavu zaidi kuwahi kurekodiwa, huku mashariki mwa Kenya ikishuhudia ukame mbaya zaidi wa msimu huo tangu mwaka 1981. Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Ukame (NDMA) imeripoti hali ya ukame katika kaunti 10, na Kaunti ya Mandera imefikia kiwango cha hatari, kutokana na uhaba mkubwa wa maji, vifo vya mifugo na kuongezeka kwa utapiamlo kwa watoto.

Hali si tofauti katika nchi jirani. Ripoti za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha hali kama hiyo nchini Somalia, Tanzania na Uganda. Tathmini ya shirika la Islamic Relief kusini mwa Somalia imebaini uhaba mkubwa wa chkula, huku zaidi ya Wasomali milioni tatu wakikimbilia makambi ya wakimbizi. Katika mji wa Baidoa, takribani asilimia 70 ya wakazi wa makambi wanaishi kwa mlo mmoja kwa siku, na watoto wengi wanaonesha dalili za utapiamlo mkali.

Wataalamu wanahusisha kwa kiasi kikubwa hali hii na mabadiliko ya tabianchi. Kuongezeka kwa joto katika Bahari ya Hindi kumesababisha dhoruba kali zaidi, huku vipindi vya ukame vikirefuka na kuwa vikali zaidi. Bara la Afrika, linaendelea kubeba mzigo mkubwa wa athari za mabadiliko ya tabianchi kutokana na miundombinu duni ya kukabiliana na majanga. Bila hatua madhubuti za kimataifa na kitaifa, mamilioni ya Waafrika wataendelea kuwa hatarini.

Support Independent Journalism

Stand With Bold Journalism.
Stand With The Standard.

Journalism can't be free because the truth demands investment. At The Standard, we invest time, courage and skills to bring you accurate, factual and impactful stories. Subscribe today and stand with us in the pursuit of credible journalism.

Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payment Kenya's most trusted newsroom since 1902

Follow The Standard on Google News

Related Topics

Ukame Drought