Na, Beatrice Maganga IEBC yafanya majaribio kuhusu mitambo ya uchaguzi Hatimaye Tume ya Uchaguzi, IEBC imeifanyia majaribio mitambo ya kutuma matokeo ya uchaguzi kwa njia ya kielektroniki katika ukumbi wa Bomas, jijini Nairobi, kituo kikuu cha kujumlisha kura. Majaribio hayo yamehusu kuyapokea matokeo kutoka vituo mbalimbali nchini ambavyo vimehusishwa katika mpango huo wa majaribio. Ni sauti ya mmoja wa maafisa wa IEBC akieleza utaratibu wa kuyapokea matokeo ya uchaguzi kutoka vituo mbalimbali vya majaribio. Matokeo hayo yalitandazwa katika mashine kubwa huku majina na picha za wawaniaji urais yakiwekwa katika mashine hiyo. Punde matokeo yanapowasilishwa na maafisa katika vituo mbalimbali kwenye kaunti, yanatandazwa katika mashine hiyo huku yakionesha idadi ya kura za kila mwaniaji. Aidha majina ya kaunti zote yameorodheshwa huku kukiwa na uwezekano wa kufuatilia matokeo ya kila kaunti kwa kubonyeza jina la kaunti inayohusika. Mwenyekiti wa IEBC, Wafula amefafanua hatua ambazo zinastahili kuchukuliwa iwapo kuna tofauti za matokeo katika mashine na yale yaliyotangazwa na afisa wa uchaguzi katika kituo. Afisa Mkuu Mtendaji wa IEBC, Ezra Chiloba aidha amesema vituo vyote vikuu vya kupeperusha matokeo ya uchaguzi vitakuwa vikipeperusha matokeo sawa huku ukiwapo wavuti maalum ambao mtu anaweza kutumia kufuatilia matokeo. Licha ya kupeperushwa kwa matangazo hayo kwa njia ya kieleketroniki wakati wa uchaguzi mkuu, Chebukati amesema kuna vituo thelathini na vitatu ambavyo matokeo yatawasilishwa kwa mfumo usio wa kielektorini kutokana na hali kwamba maeneo mengine majina ya wawaniaji zaidi yalijimuishwa dakika za mwisho kutokana na maamuzi ya mahakama hivyo majina yao hayako katika data za awali. Chebukati aidha amesema karatasi za kura kwenye maeneo mengine aidha zitachapishwa upya baada ya kujumuishwa kwa majina ya wawaniaji wengine dakika za mwisho. Kampuni za mawasiliano za Safaricom, Airtel na Telkom zitashiriki shughuli ya upeperushaji wa matokeo ya uchaguzi, tofauti na uchaguzi uliopita ambapo kampuni moja tu ya mawasiliano ilitegemewa. Hayo yanajiri huku shughuli ya kuapishwa kwa maafisa elfu mia tatu sitini watakaosimamia uchaguzi mkuu na maajenti wa wawaniaji wakiapishwa rasmi.
IEBC yafanya majaribio kuhusu mitambo ya uchaguzi
Living
By | 8 years ago | 2 Min read
.
Trending Now
- How to make choices that shape your destiny
- How do I teach my kids faith without losing their curiosity?
- Seven tips that will give you a leading edge while searching for a man
- Five bedroom secrets women want men to know
- Confessions: I infected my husband with HIV but he will never know that he got it from me
- Recipe: How to prepare Spicy chicken frittata
- Aromatherapy shower kit
- Elevate your graphic T-shirt into a fashion statement
- Experts say we've all been changing duvets wrong as they share 60-second method
- Want a more polished look? Accessories are key
.
Popular this week
- How to make choices that shape your destiny
- There is no single formula for success in marriages
- Can diet improve fertility? What science really says about it
- Untamed Foolery: Woman behind Kenya's viral EQ conversations
- Delicate dance: What reciprocity really looks like in relationships
- Easy recipe: Walnuts cheesy kunafa
- Quiet strength of mothers raising kids with special needs
- How to report a superior without risking your job
- Elevate your graphic T-shirt into a fashion statement
- Cocktail bar: The Garibaldi
.
Similar Articles
.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.