Hapo zamani za kale ma sponsor walikua ni watu wa maana sana, lakini siku hizi sijui kulifanyika nini juu ma sponsor ndio wanajileta.
Kitambo ulikua unapata mzazi ndiye anatafutia mtoto wake sponsor but siku hizi mtu anajitokeza kama sponsor juu kuna kitu anafuata.
Kitambo tulikua tunaambiwa tusome kwa bidii ndio tupate sponsor tukasomee majuu, walikua wanasponsor shule, college ama university. Lakini siku hizi sponsor wanasponsor kulipa nyumba, kununua nguo na gari na pia upkeep yote. Ni wapi kulienda vibaya sponsor wakabadilika hivyo kwa haraka?
Team mafisi wanakimbilia sponsors. Unapata jamaa ni fisi amefuata kadame size yake lakini anapata aibu anapokutana na hako kadame kakiwa na sponsor mzee kuliko baba yake. Hawa sponsors ni ma bwana za watu, baba za watu na yet anajiita sponsor — mnazoea team mafisi mbaya, juu mkiendelea hivyo, vijana wetu wenye hata sio team mafisi wataoa wapi kama mnapita na size zao?
Ndio maana nasema masponsor wacheni kuzoea team mafisi na vijana wetu.
Watu wanaanza kuongea eti, huyu jamaa amewekwa na mama mzee, mara unaskia eti jamaa ameolewa na mama mzee kuliko mama yake mpaka inakua kwa vyombo vya habari. Mara eti jamaa alishindwa kutafuta rika yake akaendea Sugar Mummy, na saa hizo jamaa ameangukia sponsor mmama venye tu madame huangukia sponsor mabuda.
kitu ningetaka ma youtman na ma youtwomen wajue ni kwamba hawa sponsors, akuwe mbaba ama mmama, time yao yakubonda raha iliisha, sasa wanawaharibia yenu kama mayout. So kaa rada na hawa masponsor juu pia unaweza pata sponsor sio wako peke yako, yani anasponsor kila mahali.
Mi naona hawa ma sponsors wamezoea team mafisi sana, juu siku hizi matotoise wameanza kukataa mavijana. Lakini kitu inanishikishanga nare ni kupata kajamaa kadogo kakiangukia sponsor mama.
Watu wa nduthi Manyanja road
Juzi kulikua na noma pale karibu na Harries along Manyanja road, ambapo majamaa wa duthi walipiga kijana mwingine mob justice eti amegonga side mirror ya nduthi na gari yake halafu akagonga vibanda kama mbili. Huyo kijana saa hizi ako kwa baba na ni juu tu ya side mirror ya piki piki. Brian Karisa Tumaini alikua tu kijana mpoa, but watu wa duthi wakammkatsia livity yake eti juu amegonga side mirror ya mmoja wao.
Watu wa piki piki mnapenda sa kujifanya eti mnajua kuchukua sheria mikononi mwenu, yet hata gari zikigongana watu hutoka na wanaskizana lakini sio kupigana mob justice.
Lazima mbehave kama watu wanatumia akili sio ni kama mnatumia makamasi kufikiria. Hamuezi kupiga mtu mpaka anakufa eti juu ya side mirror ya pikipiki. Uhai wa mtu ni kubwa kuliko hio pikipiki yako, so watu wote wa duthi tumieni akili. Na kwa Brian Karisa Tumaini, rest in peace.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national
and international interest.