×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

FBI Kushirikishwa Katika Uchunguzi wa Mauaji ya Wakili Willie Kimani

Living

Na, Carren Omae 

Nairobi, KENYA Huku uchunguzi kufuatia mauaji ya wakili Willie Kimani, mteja wake na Dereva wa texi, Shirika la Ujasusi la Marekani litashirikishwa katika uchunguzi wa maujai hayo. Kauli hii ni kulingana na Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi Nchini Ndegwa Muhoro. Muhoro ameyasema hayo alipofika mbele ya jaji Luka Kimaru leo hii. Mkurugenzi huyo aidha amesema uchunguzi huo utakamilika katika kipindi cha siku 14. Amefika kortini akiwa ameandamana na kitengo uchunguzi wa jinai Serious Crimes Prevention Unit na kile cha Flying kutoa maelezo ulikofikia uchunguzi.

Jaji huyo aidha ameagiza ripoti ya uchunguzi iliyofanyiwa mili hiyo iwasilishwe mbele ya mahakama Jumatano.

Wakati hayo yakijiri afisaa mwingine wa polisi wa utawala AP aliyetiwa mabroni kwa madai ya kuhusika na mauaji hayo ataendelea kuzuiliwa kwa siku 13. Kukamatwa kwa afisa huyo kunafikisha wanne idadi ya maafisa waliotiwa mbaroni kufuatia mauaji hayo. Hakimu Mkuu wa mahakama ya Milimani Joyce Gandhani ameagiza Sergeant Leonard Maina Mwangi kuzuiliwa katika kituo cha polisi kisichojulikana ili kutoa nafasi kwa uchunguzi zaidi kufanywa.

Afisaa wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma DPP, Duncan Ondimu aliiagiza mahakama kumzuilia mshukiwa kwa misingi kwamba huenda akaingilia shughuli ya uchunguzi. Amesema Ofisi ya DPP imebuni kamati maalum itakayoshirikiana na maafisa wa polisi kufanya uchunguzi wa mauaji hayo.

Kuzuiliwa kwa afisa huyo kunajiri siku moja tu baada ya maafisa wengine watatu Fredrick Leliman, Stephen Chebulet na Silivia Wanjiku, waliohusishwa na mauji hayo kuzuiliwa kwa siku 14.

Kimani mteja wake Josephat Mwenda, n dereva wa Texi Joseph Muiruri walitoweka tarehe 23 mwezi Juni kisha wakapatikana wakiwa wameuliwa siku chache baadaye.

 

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles