Jameni tumeingia msimu wa sikukuu tupende tusipende , na msimu huu huja na mwembwe na mahanjam yake sio haba.
Ni wakati huu ndio utapata watu wakiwa na tabia za kushangaza mno , tabia ambazo hujitokeza tuu msimu huu.Sijui kama ni pupa , au ni msisimko wa kupindukia bali tabia za kina yakhe wengine huwa za udhi kweli!