Wavuvi 54 kutoka taifa jirani la Tanzania wanashughulikiwa na Idara ya Uhamiaji

Wavuvi 54 wa kigeni waliokuwa wakiendeleza shughuli za uvuvi katika ufuo wa bahari wa Pemba nchini Tanzania ambao walizidiwa na mawimbi makali ya bahari na kujipata katika bandari ya Old Ferry Kilifi mapema jana, kwa sasa wanashughulikiwa na Idara ya Uhamiaji.

Kamishna wa Kaunti ya Kilifi, Magu Mutundika amesema juhudi zinawekwa ili kuhakikisha wanarejea nchini mwao salama ikizingatiwa hawana stakabadhi za kuwaruhusu kuwa humu nchini. Hamadi Haji Juma, mmoja wa wavuvi hao amsema kwamba mawimbi makali ya bahari yalisababisha kuharibika kwa mashua yao.

Hayo yanajiri huku Mwenyekiti wa Muungano wa Wavuvi katika Kaunti ya Kilifi, Shallo Issa akisema kwamba jumla ya mashua 15 za uvuvi zimewasili kwenye fuo mbalimbali za bahari ukiwamo ule wa Uyombo, Mtwapa na Ngomeni baada ya kukubwa na mawimbi makali.

Related Topics

tanzania fishermen