shughuli ya kutoa mafunzo kwa walimu kuhusu mtalaa mpya yafaulu pakubwa

Waziri wa Elimu, Prof George Magoha ametangaza kwamba shughuli ya kutoa mafunzo kwa walimu kuhusu mtalaa mpya ilifaulu pakubwa huku  walimu elfu 91 wakipewa mafunzo hayo.  Akizungumza mjini Kisumu, Magoha amewakosoa wale wanaopinga mafunzo kwa walimu japo amesema yu tayari kushiriki mazungumzo zaidi na washikadau mbalimbali.

Hata hivyo amesema kamwe hatakubali mpango huo kusambaratishwa na watu wachache, kwani tayari hatua kadhaa zimepigwa kukiwamo kutengwa fedha za kutosha kwa shughuli yenyewe.

Mafunzo hayo yaliyoanza Jumanne kwenye sehemu mbalimbeli nchini yanakamilika leo.

Hapo jana akiwa kwenye Kaunti ya Kisii, Magoha alitoa hakikisho kwamba serikali imetenga fedha ili kufanikisha uboreshaji wa miundo msingi katika kila shule nchini. Aliahidi kwamba mafunzo hayo yataendelea kwa awamu ya pili kupitia mfumo wa kidijitali wakati shule zitakapofunguliwa kwa muhula wa pili.

Related Topics

mtalaa mpya