Kiunjuri asutwa kwa kuchelewa kuwasilisha ripoti ya jopo lililoteuliwa na Rais

Naibu mwenyekiti wa jopo liloteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta,  kushughulikia changamoto za wakulima  wa mahindi Patrick Khaemba amemsuta mwenyekiti wa jopo hilo ambaye pia ni Waziri wa Kilimo,  Mwangi Kiunjuri kwa kuchelewa kuwasilisha  ripoti ya jopo hilo kwa Rais Kenyatta.

Khaemba ambaye  ni Gavana wa Kaunti ya Trans Nzoia, amesema wakulima ambao wanaendelea kuyatayarisha mashamba yao tayari kwa upanzi wamejipata kwenye  njia panda wasijue mstakabali wa sekta hiyo ya kilimo.

Haya yanajiri wakati ambapo foleni ndefu bado zinashuhudiwa katika Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao, NCPB wakisubiri kuyawasilisha mahindi kutokana na masharti iliyowekwa na Wizara ya Kilimo lengo likiwa kuwazuia mawakala kuyawasilisha maindi.

Alexander Agui ni mkulima Kaskazini mwa Bonde la Ufa.

Ikumbukwe mwaka uliopita wakulima walivuna takribani magunia ya mahindi milioni 46 ya kilo tisini na serikali ilihaidi  kuyanunua magunia milioni mbili pekee huku wakulima wa Kaunti ya Uasin Gishu wakisaini mkataba na kampuni ya ETG kuyanunua mahindi yao na kuwauzia mbolea kwa bei isiyozidi shilingi elfu 3.

Related Topics