Shirika la Habari la Standard linalenga kuendeleza ushirikiano wake kupitia mkataba na serikali ya kaunti ya Uasin Gishu kufanikisha Makala ya pili ya mbio za Eldoret City Marathon zitakazoandaliwa tarehe 21 mwezi Aprili 2019

Shirika la Habari la Standard  linalenga kuendeleza ushirikiano wake kupitia mkataba na serikali ya kaunti ya Uasin Gishu kufanikisha Makala ya pili ya mbio za Eldoret City Marathon zitakazoandaliwa tarehe 21 mwezi Aprili.

Afisa Mkuu mtendaji wa shirika hili Orlando Lyomu, ameahidi kuendelea kuwapo kwa ushirikiano huo kwa lengo la kufanikisha mbio  hizo zenye maazimio ya kutunza mazingira.

Shirika la Habari la Standard  linalenga kuendeleza ushirikiano wake kupitia mkataba na serikali ya kaunti ya Uasin Gishu kufanikisha Makala ya pili ya mbio za Eldoret City Marathon zitakazoandaliwa tarehe 21 mwezi Aprili.

Akizungumza wakati wa hafla iliyowaleta pamoja wafadhili wa mbio hizo nje ya afisi ya Gavana Jackson Mandago, Afisa Mkuu mtendaji wa shirika hili Orlando Lyomu, ameahidi kuendelea kuwapo kwa ushirikiano huo kwa lengo la kufanikisha mbio  hizo zenye maazimio ya kutunza mazingira.

Haya yakiwa Makala ya pili ambapo shirika la Standard limefadhili likiwa mdhamini mkuu, zaidi ya miche elfu hamsini imepandwa, hatua ambayo imepongezwa na Orlando.

Ikumbukwe  shirika la Standard  limekuwa kwenye harakati za kuwafikia wakenya katika maeneo mbalimbali nchini kupitia kuweka mikataba na serikali za kaunti.

Mwezi uliopita, Orlando aliongoza kikosi cha Shirika hili kuweka mkataba na serikali ya Kaunti ya Elgeyo Marakwet kuhusu mbinu za kuboresha kilimo kupitia vipindi vya mafunzo ya kilimo kwenye runinga ya KTN Farmers.

Shirika la Habari la  Standard, limetia saini mkataba wa ushirikiano na Benki ya Equity ikiwa ni njia mojawapo ya kuimarisha mauzo yake tarehe Machi 20

Katika hafla iliyofanyika  katika Makao Makuu ya shirika hili kwenye Barabara Kuu ya Mombasa, Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika hili Orlando Lyomu , amesema ushirikiano huo utaimarisha biashara na kuwapa uwezo wa kiuchumi wasambazaji wa magezeti.

Orlando aidha amesema kwamba mkataba huo utaboresha zaidi mazingira ya kufanya biashara kati ya wadau hawa wawili huku ukilenga zaidi kuwanufaishi wahudumu wa magezeti.

Naye Meneja Mkurugenzi wa Benki ya Equity Polycarp Igathe, amepongeza ushirikiano mwema wa Kampuni ya Standard na washikadau wengine, akifichua kwamba benki hiyo inalenga kubuni nafasi za kazi kupitia utoaji mikopo kwa wasambazaji wa magezeti. Igathe vilevile amesema wahudumu hao kamwe hawatahitaji mdhamini wa kupokea mikopo hiyo.

Related Topics

Mkataba Standard