Usalama umeimarishwa kwenye Kaunti ya Mandera kufuatia jaribio la Al Shabaab kuivamia kambi moja ya GSU

Beatrice Maganga,

Usalama umeimarishwa kwenye Kaunti ya Mandera kufuatia jaribio la washukiwa wa kundi gaidi la Al Shabaab kuivamia kambi ya maafisa wa GSU ya Dabacity usiku wa kuamkia tarehe 26, Februrari mwaka huu.

Mmoja wa maafisa wa polisi waliwaona washukiwa hao wakiikaribia kambi hiyo hali iliyochangia ufyatulianaji wa risasi.

Kamanda wa Polisi kwenye eneo la Kaskazini, Paul Soi amesema hakuna afisa aliyejeruhiwa wakati wa makabliano hayo. Uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea. 

SEE ALSO :Islamist bomb targets Mogadishu hotel, killing at least 10

Register to advertise your products & services on our classifieds website Digger.co.ke and enjoy one month subscription free of charge and 3 free ads on the Standard newspaper.

Al ShabaabUsalamaMandera