Watu 84 wafariki dunia India kwa kunywa pombe yenye sumu

Watu 84 wamefariki dunia na wengine 200 kulazwa baada ya kunywa pombe yenye sumu nchini India.

Inaarifiwa waathiriwa ni wafanyakazi wa shamba la majani chai eneo la Assam. Wiki mbili zilizopita watu wengine mia moja walifariki dunia dunia kutokana na kisa sawa na hicho

Inahofiwa kwamba huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka. Madaktari nchini humo wanasema waathiriwa walifika hospitalini wakiwa na maumivu makali ya tumbo, kifuo na kushindwa kupumua vizuri.

Nchini India kuna visa vingi vya utengenezaji wa pombe haramu. Kwa sasa jopo kazi maalum limebuniwa kuchunguza vifo hivyo.