Mahakama ya Juu imedumisha ushindi wa Gavana wa Laikipia na Mbunge wa Shinyalu

Gavana wa Liakipia Nderitu Muriithi na Mbunge wa Shinyalu Justus Kizito wamepata afueni katika mahakama ya juu baada ya kesi zilizokuwa zikipinga ushindi wao kutupiliwa mbali. Katika kesi ya kwanza, Jaji Smokin Wanjala, amekataa madai ya mpinzani wa Gavana Muriithi Sammy ndung'u kwmaba kulikuwapo na udanganyifu wakati wa uchaguzi Mkuu wa Agosti mwaka 2017. Aidha amesema mlalamishi hakuwasilisha ushahidi wa kutosha kuiwezesha mahakama kutupilia mbali ushindi huo.

Hii ni mara ya tatu kwa Muriithi kudumisha ushindi wake kufuatia maamuzi ya mahakama. Awali Mahakama Kuu na ile ya Rufa ailitupilia mbali kesi iliyokuwa ikipinga ushindi wa Gavana kufuatia misingi hiyo hiyo.

Katika uamuzi, mahakama hiyo imesema hazikuwapo sababu za kutosha za kufutilia mbali ushindi wa mbunge wa Shinyalu. Kesi ya kupinga ushindi wa munge huyo iliwasilishwa na Silvester Anami, kwa misingi kwamba uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu.

Baada ya Kizito kushinda katika uchaguzi wa Agosti mwaka 2017, Anami aliwasilisha kesi katika Mahakama Kuu japo kesi yake ilitupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi na kuagizwa alipe shilingi milioni tano gharama ya kesi.

Aidha, aliwasilisha rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu japo rufaa hiyo pia ilitupiliwa mbali.

Related Topics

Nderitu Shinyalu