Ilhan aliishi katika kambi la wakimbizi ya Dadaab humu nchini

Uchaguzi wa kati ya muhula ukikamilika Marekani Mwanamke wa miaka 36 Ihlana Omar ametaeuliwa kuwa mwanamke wa kwanza wa asili ya Kisomali na wa kwanza wa dini dini ya Kiislamu kuchaguliwa katika bunge la Congress nchini humo.

Ihlana ambaye alikuwa mkimbizi baada ya vita kuibuka Somalia aliishi katika kambi la wakimbizi ya Dadaab humu nchini na familia yake kuanzia mwaka wa 1991 hadi 1995 kabla ya kuhamia Marekani, atawakilisha eneo la Minnesota, Minniapolis.

Ilhan amechaguliwa pamoja na Rashida Tlaib, hivyo kuwa wanawake wawili wa kwanza waislamu kuchaguliwa katika bunge hilo.

Ihlan atachukua hatamu kutoka kwa Keith Ellison ambaye likuwa Muislamu wa kwanza kuchaguliwa katika Congress.

Mwaka wa 2016 alichaguliwa kuwa Mbunge wa kwanza wa alisi ya Kisomali kuwakilisha eneo la Minniapolis.