The Standard Group Plc is a
multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper
print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key
influence in matters of national and international interest.
NASA yasema itakwenda mahakamani kupinga matokeo ya urais
Kivumbi cha matokeo ya urais sasa kinatarajiwa kutifuliwa mahakamani. Siku nne baada ya Tume ya Uchaguzi, IEBC kumtarangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi, hatimaye Muungano wa NASA umeafikia uamuzi wa kuwasilisha kesi katika Mahakama ya Juu kupinga matokeo hayo. Katika kikao kilichohudhuriwa na vinara wa muungano huo, Raila Odinga, Musalia Mudavadi na Moses Wetangula, muungano huo umesema una ushahidi wa kutosha kuonesha kwamba ulikuwapo udanganyifu mkubwa wa kumpendelea Kenyatta, huku ukiwashtumu baada ya waangalizi.
Katika tangazo hilo lililosubiriwa kwa hamu, Kinara wa NASA Raila Odinga alianza moja kwa moja kulalamikia mtindo anaodai umekuwapo kwa muda sasa, wa kuwatangaza washindi watu ambao hawakuchaguliwa na wananchi kidemokrasia.
Raila ameishtumu vikali Tume ya IEBC kwa kuanza kupeperusha matokeo katika wavuti wake, hata kabla ya kuzipokea fomu za kuyathibitisha matokeo.
Aidha NASA imeibua madai ya kuwapo vituo na makarani bandia kwa lengo la kufanikisha udanganyifu huo na kuilaumu IEBC kwa kupuuza malalamishi yao, badala yake kuharakisha kutangaza matokeo hayo.
Raila amesema matokeo yaliyotolewa na IEBC yalilitokana na ukarabati wa komyuta.
Waangalizi wa uchaguzi ambao walikuwa wakiwashinikiza NASA kukubali matokeo hata kabla mshindi rasmi wa uchaguzi kubainika vilevile wameshtumiwa vikali.
Raila vilevile amekosoa vikali ukandamizaji wa mashirika ya Africog na KHRC akisema ni lengo la kuyazuia kuwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo ya urais. Vilevile ameshtumu dhuluma za maafisa wa usalama dhidi ya wafuasi wake.
Ameisihi jamii ya kimataifa na wapigainiaji wa demokrasia barani Afrika kujiunga nao katika harakati za kutafuta haki.
Ikumbukwe muda wa kuwasilisha kesi kupinga ushindi wa urais utakamilika Ijumaa wiki hii.
Kulingana na sheria za Kenya, kipengele cha tisa cha katiba ibara ya 140 kinachohusu uhalali wa uchaguzi wa urais, wasioridhishwa na matokeo hayo wana kipindi cha siku saba baada ya mshindi kutangazwa, kuwasilisha kesi katika Mahakama ya Juu. Mahakama hiyo kisha itakuwa na kipindi cha siku kumi na nne kusikiliza malalamishi yaliyoibuliwa na hatimaye kufanya uamuzi. Iwapo utakuwapo ushahidi wa kutosha kufutulia mbali uchaguzi, shughuli hiyo itarudiwa katika kipindi cha siku sitini.
Ikumbukwe Mahakama ya Juu ina majaji saba wa kusikiliza kesi hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Jaji Mkuu, David Maraga, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mbete Mwilu, majaji Jackton Boma Ojwang, Smokin Wanjala, Njoki Susanna Ndung'u na Isaac Lenaola.
Premium Article
Get Full Access for Ksh299/Week.
Uncover the stories others won't tell. Subscribe now for exclusive access.
Stand With Bold Journalism.
Stand With The Standard.
Journalism can't be free because the truth demands investment.
At The Standard, we invest time, courage and skills to bring you accurate,
factual and impactful stories. Subscribe today and stand with us in the
pursuit of credible journalism.