Watoto walio chini ya miaka mitano kupata chanjo dhidi ya polio

Na Mate Tongola
NAIROBI, KENYA, Zaidi ya watoto milioni tatu walio chini ya umri wa miaka mitano katika kaunti kumi na tano watachanjwa dhidi ya ugonjwa wa kupooza, polio, kuanzia wiki ijayo.
Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema hatua hiyo inalenga kudhibiti visa vya maambukizi nje ya mipaka ya Kenya. Chanjo hiyo itaanza kutolewa Jumatano hadi Jumamosi baada ya kuzinduliwa katika Hospitali ya Rufaa ya Isiolo.
Hatua hiyo inajiri baada ya ripoti ya utafiti wa kila miezi mitatu ya wizara hiyo kubainisha kuwa kaunti za Nairobi, Lamu, Tana River, Garissa, Wajir, Mandera, Marsabit, Isiolo, Samburu, Turkana, Pokot Magharibi, Trans Nzoia, Uasin Gishu, Bungoma na Busia zinakabiliwa na hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo.

 

Related Topics