Please enable JavaScript to view advertisements.
×
App Icon
The Standard e-Paper
Join Thousands Daily
★★★★ - on Play Store
Download App

Askofu Wabukala asema anatosha kuongoza EACC

Na Mate Tongola
Wakenya wanne wamewasilisha waraka wa kupinga uteuzi wa Askofu mstaafu Eliud Wabukhala kuwa Mwenyekiti mpya wa Tume ya ufisadi EACC. 
Wanne hao; Kasisi John Mbugua, Gilbert Mukabane, Eric Abu na Jeramba Munuhe wanadai kwamba Wabukhala alifeli katika utendakazi wake hivyo hastahili kuhudumu katika EACC.
Katika waraka waliowasilisha bungeni wakati wa kikao cha kumhoji Wabukhala kilichoongozwa na Kamati ya Sheria na Haki ya Bunge la kitaifa, wanne hao wamemshtumu kwa kuwabatiza na hata kuwazika wahalifu jambo ambalo ni kinyume na maadili ya kikristo.
Hata hivyo akijitetea, Wabukhala amesema ni jukumu la viongozi wa dini kutangamana na wenye dhambi ili kuwapa muongozo. Kamati hiyo ilimtaka kuelezea kuhusu mabadiliko atakayoteka katika EACC.  
Kamati hiyo itawasilisha ripoti yake kuhusu Wabukhala katika Bunge la Kitaifa tarehe kumi na saba mwezi huu wakati wa kikao maalum kilichoitishwa na Spika Justin Muturi.
Wadhifa wa mwenyekiti wa EACC uliachwa wazi kufuatia kujiuzulu kwa Philip Kinisu baada ya kuhusishwa na ufisadi.
Premium Article

Get Full Access for Ksh299/Week.

Fact-first reporting that puts you at the heart of the newsroom. Subscribe for full access.
Continue Reading  →
What you get
  • Unlimited access to all premium content
  • Ad-free browsing experience
  • Mobile-optimised reading
  • Weekly newsletters & digests
Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payments Kenya's most trusted newsroom since 1902
Support Independent Journalism

Stand With Bold Journalism.
Stand With The Standard.

Journalism can't be free because the truth demands investment. At The Standard, we invest time, courage and skills to bring you accurate, factual and impactful stories. Subscribe today and stand with us in the pursuit of credible journalism.

Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payment Kenya's most trusted newsroom since 1902