Je, Marekani alihusika katika kifo cha ghafla cha Rais Morsi?

Aliyekuwa Rais alochaguliwa kihali kule Misri Mohammed Morsi.

Kifo cha ghafula cha aliyekuwa Rais alochaguliwa kihali kule Misri Mohammed Morsi juma lilopita katika mahakama kimewashtua wengi na kuacha maswali mengi.

‘Kwa niaba ya watu wa Uturuki tunatowa risala za rambi rambi kwa familia ya Morsi kwa kifo chake’ asema Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na kumlaumu mtawala wa sasa wa Misri Abdel Fattah El-Sisi kwa masaibu na kifo cha Morsi.

Kiongozi mwengine mashuhuri alotowa rambi rambi zake ni kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani aliyemtaja Morsi kama alokufa kama shahid (martyr). Ilikuwa Jumane taehe 17 Juni 2019 wakati Morsi alipoletwa mahakamani kwa kesi ya ‘uhaini’.

Hii ilikuwa moja ya mahangaiko alopata Morsi akiwa amefungwa jela tangu miaka sita iliyopita. Ni wakati alipotaka kujitetea akiwa amewekwa katika chumba cha kioo ndipo alipoanguka na kufa akipelekwa hospitali.

Dhuluma kubwa ni kuwa serikali ya kijeshi ya Abdel Fattah El-Sisi ilikataa kumpa haki ya kujitetea katika tuhuma alopewa. Tukumbuke Mohammed Morsi akiwa kiongozi wa Muslim Brotherhood alishinda kura za kwanza huru Misri tena kwa kura nyingi.

Hatahivyo, baada ya mwaka mmoja tu ElSisi akishirikiana na nchi za kimagharibi hususan Marekani na Israeli zilifanya njama na kumpendua. Tukumbuke huyu El-Sisi alifunzwa kijeshi kule Marekani ambapo alikuzwa ili achukuwe uongozi ambao utaelewana na Marekani.

El-Sisi alimfunga Morsi katika jela ya kijeshi ya ‘Tura’ ambapo aliteswa usiku na mchana huku akinyimwa matibabu na hata kukutana na jamaa zake. Katika mapinduzi hayo dhidi ya Morsi mwaka 2013 El-Sisi aliamuru kunyongwa kwa viongozi na wafuasi wa Morsi zaidi ya 50.

Cha kushangaza ni kuwa mataifa ya kimagharibi na hasa Marekani hawakulani mauaji haya bali walizidi kumpa msaada wa hali na mali Dikteta wao El-Sisi. Yamkini utawala wa Morsi haukuwavutia wamagharibi kwani alienda kinyume na falsafa yao ya ukandamizi kinyume na imani za dini. Akiwa Rais Morsi alipinga ubepari na kutawala kwa misingi ya kidini.

Alilaumu utawala wa Syria kwa kuwaua raia kiholela. Morsi pia alilaumu taifa la Israeli kwa kuwagandamiza wapalestina katika makao yao haswa Gaza.Alitaka suluhisho la kudumu kwa tatizo la mayahudi na wapalestina. Kutokana na sera zake hizi mataifa ya magharibi, Israeli na washirika wake walipanaga njama za kumuondowa na kumweka kibaraka. Kupitia kwa El-Sisi alokuzwa Marekani majeshi walimpendaua, kumfunga na kumtesa Morsi bila sababu ya maana bali uzushi.

Swali ni itakuwaje kumfungulia mashtaka Rais alochaguliwa kidemokrasia? Je, kosa la Morsi lilikuwa lipi? Na ushahidi ulikuwa upi? mbona haki haikutumika kuita mashahidi na Morsi kuwa na wakili? Lilikuwa jambo la kusikitisha kumfungia Morsi jela kwa miaka sita korokoroni.

Huu ni unyama wa hali ya juu na kinyume cha haki za binadamu. Sambamba na maelezo ya mfuasi wa Morsi kwa jina Muhammad Sudan alohojiwa katika runinga ya Al-Jazeera yasemekana Morsi alikuwa anateswa jela kila mara.

Alikatazwa kuwaona jamaa zake na pia alilazimishwa kulala sakafuni ambalo aliathirika kiafya.Hakuruhusiwa kupata matibabu na aliteswa. Baada ya kifo chake akipelekwa hospitali utawala wa El-Sisi uliharakisha mazishi yake huku familia yake ya karibu ikiruhusiwa kuhudhuria na wafuasi wake kukatazwa na hata waandishi habari.

Watetezi wa haki wanashuku uwezakano kuwa serikali ya Misri huenda ilimdhuru na kupelekea kifo chake ama kwa kumtesa? Shaka hii inadhihuri kwa siri kubwa ya kuharakisha kuzikwa kwa mwili wa Morsi.

Je, wanaficha ushahidi wa kifo chake? Kwanini kumzika kimyakimya na hali ni mtu wa watu aliye mashuhuri? Katika ujumbe wake katika ukumbi wa jamii wa uso wa kitabu yaani ‘Facebook’ mwana wa kiume wa Morsi kwa jina Ahmad alisikitishwa na kifo cha babake.

‘Baba lala salama tutakutana katika ukumbi wa Allah kesho ahera’Ahmad alisema na kuongeza kuwa malipo yako kesho na wahusika watalipwa tu. Uongozi wa El-Sisi umekithiri kwa ukatili mkubwa kwani maelfu wa wafuasi wa vuguvugu la kiislamu la ‘Muslim Brotherhood’ wananyongwa kama kuku na utawala huu wa kidekteta.

Morsi ni kiongozi ambaye alikuwa anapendwa na aliwasaidia wanyonge. Hakupenda makubwa na hata alikataa mshahara mkubwa wa Rais na kuridhika na mshahara wa wastani, Yasemekana Morsi alikataa kukaa katika ikulu ya Rais na kuridhika kukaa pamoja na wananchi mtaani ambapo alifurahia kuswali nao pamoja.

Shani nyingine ya Morsi ni kuwa alikataa picha yake kuanikwa katika ofisi za serikali na badala yake akaamuru maandishi ya kumsifu Mungu kuwa ni mkubwa yaani ‘Allahu Akbar’. Ni wazi El-Sisi alimuona Morsi kuwa tisho kwa utawala wake na alipanga kumuangamiza.Je, ni kwanini El-Sisi atake kumuangamiza Morsi ?

Sambamba na hali halisi ilojitokeza ni wazi El-Sisi alikuwa anatumiwa kama kibaraka wa Marekani dhidi ya wanaopinga sera zake kama Morsi.

Kumfunga bila kumaliza kusikizwa kwa mashtaka dhidi ya Morsi ni kuenda kinyume na haki. Ni unyama mkubwa kwa El-Sisi kumuweka Morsi katika kichumba cha kioo kama ndege na kumnyima haki ya kujitetea.