Kiwanda cha kutengeneza vileo cha Keroche kinatarajiwa kufunguliwa leo hii. Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi KRA itaongoza hafla ya kukifungua kianda hicho mjini Nakuru.
Hatua hii inafuatia uamuzi wa Mahakama ya Juu iliyoiagiza KRA kukifungua kiwanda hicho hadi kesi iliyowasilishwa na Afisa Mkuu Mtendaji Tabitha Karanja itakaposikilizwa na kuamuliwa.