Manchester City inasubiri droo ya leo bado ya kuilaza Steau Bucharest bao moja kavu

Na,Hassan Ali

Hebu tuangazia kidogo baadhi ya matokeo ya mechi za klabu bingwa barani Ulaya zilizopigwa hapo jana usiku. Man City imeingia hatua muhimu ya makundi ikisubiri droo ya leo baada ya kuilaza Steau Bucharest bao moja kavu. Bao la washindi limetiwa kimiani na Fabian Delph. Rostov nayo imevuna ushindi mnono wa mabao 4 kwa 1 dhidi ya Ajax. Droo ya mechi za makundi itaandaliwa leo jioni kwenye milango ya saa moja usiku. Uingereza itawakilishwa na timu nne ambazo ni bingwa mtetezi Leicester, Arsenal, Man City na Tottenhem Hotspurs.