×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Maisha peupe: Uoga ndiyo adui mkubwa maishani

News
 uoga husababisha mtu kutopiga hatua zozozote maishani Picha: Hisani

Je wajua kuwa watu wengi katika ulimwengu huu wamefeli maishani sio kwa kuwa ni wapumbavu au wajinga lahasha bali wamekosa kuafikia mengi maishani kwa kuwa na uoga wa aina fulani?

Hilo nalisema bila uoga wala tashwishi kwani katika fani hii ya uanahabari nimekutana na watu wa tabaka mbali mbali na kati ya hawa nikagundua kuwa wengine wamekumbwa na uoga wa jambi mmoja au jengine.

Kwa mfano utapata kwamba kuna watu ambao hushindwa kutoa maoni yao mbele ya watu — kimoyomoyo wanadhani kuwa maoni yao hayafai au hata ni bure kabisa.

Wengine nao hawawezi kudhubutu kuuliza swali kwani wanadhani kuwa maswali yao ni ya kipumbavu. Maswala haya mawili yanaashiria uoga na uoga huo ndio huwa kizingiti kikubwa kwa watu wengi.

Kuna aina mbali mbali za uoga ambazo huadhiri watu. Wengi huwa na uoga wa kukataliwa (rejection) — hii inamaanisha kuwa afadhali asije akaomba kazi au hata kumchumbua mtu iliasije akakataliwa.

Woga huo humfanya mtu aishi maisha ya upweke na kuhisi kana kwamba yuko jela.

Uoga mwengine ni ule wa kukataa mabadiliko. Kwa mfano mabadiliko maishani hukuja wakati mmoja au mwengine na kuna watu ambao hawapendi mabadiliko, yawe ni ya kikazi, serikalini au hata maisha yao yenyewe. Pia kuna uoga wa kuwachwa mpweke.

Hii inamaanisha kuwa watu wengine hawawezi kukata kauli maishani pasipo maoni ya watu wengine. Yaani wao wanasubiri maoni ya wenzao ili waamue mwelekeo wao.

Aina hii ya uoga husababisha mtu kutopiga hatua zozozote maishani na wanahisi kana kwamba wanazunguka zunguka bila mwelekeo.

Njia mzuri ya kumaliza uoga maishani ni kwa kujikubali ulivyo, na pia kuchunguza na kurekebisha kinachokukosesha usingizi.

Baadhi ya mibabu ambao wamefaulu duniani kwa fani mbalimbali ni watu ambao walipiga moyo konde na kufahamu fika kuwa uoga ingawaje upo, hawataangazia uoga bali wataangazia swala likubwa kuliko uoga.

Kumbuka hatima ya uoga ni kuishi maisha kana kwamba uko gerezani. Amua leo kuishi maisha ya ujasiri.

Wasiliana nami [email protected];

Facebook: Anne Njambi Ngugi;

Twitter: @annngugi

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles