Kamati Maalum Kubuniwa ili kuthibiti mchezo wa kamare

Na ,carren Omae

Kamati Maalum Kubuniwa ili kudhiti mchezo wa kamare
Huku idadi ya Wakenya wanaoshiriki mchezo wa bahati nasibu yaani Betting ikiongezeka nchini, Bunge la Taifa linapendekeza kubuniwa kwa kamati maalumu itakayothibiti mchezo huo. Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Adan Duale, amesema kamati hiyo itaangazia jinsi biashara hiyo inavyoendeshwa nchini, uhalali wake, wamiliki na iwapo wanalipia kodi ipasavyo.
Akiwasilisha mswada huo katika kikao cha bunge cha alasiri, Duale amelalamikia visa ambapo wanafunzi walio na umri wa chini wamekuwa wakijihusisha na mchezo huo suala ambalo amesema linaathiri shughuli zao za masomo.
Wabunge wengi waliochangia wameunga mkono kauli ya Duale huku wakisema huenda wengi wa wamiliki wamekuwa wakikwepa sheria hasa kuhusu ulipaji kodi na kuna haja ya kuthibitiwa.
Mbunge wa Budalangi Ababu Namwamba amesema wengi hasa wanafunzi wamekuwa waraibu wa mchezo wa betting, jambo ambalo huenda likaathiri jamii siku zijazo.
Mswada huo unatarajiwa kuwasilishwa rasmi bungeni ili kujadiliwa.