JSC Yakosolewa kwa Kutojibu Masuali Kuhusu Uteuzi wa Jaji Mkuu Mpyaa

Na, Beatrice Maganga

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Nchini, Yash Pal Ghai ameishtaki Tume ya Huduma za Mahakama JSC kwa kutoziweka bayana sababu za kukatowaorodhesha baadhi ya watu waliowania nyandifa kwenye idara ya mahakama zilizotangazwa hivi majuzi. Kupitia wakili wake Waikwa Wanyoike, Ghai amesema kuwa licha ya kuiandikia barua tume hiyo mnamo Julai 14, hadi sasa hajapokea maelezo.
Amesema hatua hiyo inakiuka katiba inayosisitiza umuhimu wa uwazi vilevile uongozi bora serikalini. Ghai pamoja na mkenya kwa jinar Samwel Muhochi wameitaka mahakama kuiagiza JSC kuweka wazi sababu hizo kwa umma. Mahakama imeitaja kesi hiyo kuwa ya dharura na kuagiza isikilikwe siku ya Ijumaa wiki hii.
Tume hiyo ilizitangaza nafasi za Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na Jaji kwenye mahakama hiyo mnao Juni kumi na saba. Tume hiyo kisha iliyaorodhesha majina ya wawaniaji wa nafasi hizo kati ya Juni 14 na 21 kabla ya kuwateua baadhi yao. Msomi Makau Mutua ni miongoni mwa waliotemwa kwa wanaowania nafasi ya Jaji Mkuu. Walioteuliwa wataanza kuchujwa Agosti 29 hadi Oktoba 7.

 

Related Topics