Tusiwadhulumu waume zetu

Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia dhuluma wanazozipitia wanaume mikononi mwa wake zao katili. Hivi majuzi mwanaume mmoja kajipata matatani baada ya sehemu yake nyeti kukatwa. Kisa kingine cha hivi majuzi inatamausha kwani mwanamke mmoja kamchoma kisu mpenziwe mgongoni na pia kinena chake.Visa vingi vya aina hii inakera moyo ikizingatiwa kuwa inaenda kinyume na mantiki ya kibinadamu.

Wasemavyo weledi wa  lugha, aliyeumwa na nyoka akiona ung’ong’o hushtuka.Ukweli wa kauli hii unadhihirika katika jamii zetu pale ambapo wanaume wameasi majukumu yao ya kifamilia ili kukwepa dhuluma watakazokumbana nazo.Takwimu zinaonyesha kuwa dhuluma za aina hii huchangia pakubwa na ndio msingi wa kuvunjika kwa ndoa. Aidha huwaathiri watoto ikikumbukwa kuwa wanahitaji uzazi mwema kutoka kwa wazazi wao.

 Inasikitisha mno kuona waathirika kunyamaza pasi na kueleza dhiki wanayopitia. Wao huhofia kudharauliwa na rafiki zao na pia fedheha watakayopata hadharani ikijulikana kuwa wake zao huwadhulumu.Yafaa wanaodhulimiwa kiziziba nyufa ili ndoa zao isije ikasambaratika. Wa aidha wasije wakajutia kuta zitakapoporomoka.

 Ijapokuwa wanaume hujihusisha katika uraibu wa ulevi,uzinifu na mafarakano yasiyoeleweka, inabidi wanawake kuchukua jukumu la kutafuta suluhusho la kudumu ama njia mbadala  kukabiliana na waume zao pasi na kuwadhulumu visivyo.Ushauri nasaha kwa familia zinazozozana ni njia ifaayo kukwepa dhuluma ili kuleta maridhiano na uwiano.

  Wanawake wanapaswa kuwakabidhi waume zao hadhi wanayostahili pasi na kuwadunisha hadharani. Hali kadhalika watatue shida zao za kifamilia bila kuangazia matatizo yao hadharani.