Wanawake na mavazi. Je unapomuona mwanamke ama msichana yeyote, jambo la kwanza ambalo huwa waangalia ni nini? Ni mavazi au ni nywele ama ni vipodozi? Na iwapo huyu mwanamke anataka kuwa kiongozi kwa mfano, utamhukumu na nini ukimwona kwa mara ya kwanza? Mavazi? Ni majeli yake (maumbile) ama utangoja azungumze? Kwa kweli sisi wanadamu tunao uzoefu wa kuwahukumu wenzetu kwa maumbile yao ya nje tu kabla ya jambo jingine lolote.
Ukipatana na mtu yeyote utamwangalia na kum? kiria kwa namna fulani kulingana na vile alivyovaa. Basi jambo hili linawaathiri wanawake kwa sana kuwaliko wanaume. Leo acha tuongee kuhusu mavazi hasa ya wanawake na wasichana uongozini. Je mavazi yana umuhimu upi katika mwanamke anayetaka kuwa kiongozi, sharti avae nguo fulani? sharti awe na nywele fulani na uso wake kupakwa mafuta kwa jinsi fulani? Hili ni swali nililowauliza vijana wenzangu tulipokuwa tunapiga gumzo pale mtaani.